Sauti ya Amerika  Swahili
Pata habari za kuaminika

Kwa Maandishi Pekee
Search

VOA Swahili Service Banner (Image source: AP Photo from U.S. State Department))

Tangu mapema mwaka huu idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Amerika  ina matangazo ya nusu saa ya alfajiri  na ya mchana kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Matangazo ya alfajiri - "Kumekucha Afrika" husikika kuanzia saa kumi na mbili alfajiri saa za Afrika ya Mashariki. Na "Dira ya Afrika" ni matangazo yanayo sikika hapo saa sita na nusu za mchana saa za Afrika Mashariki. Matangazo ya jioni ni yale yale ya saa nzima kuanzia saa moja unusu usiku. 

Matangazo ya Jumamosi na Jumapili, husikika pia kwa saa nzima kuanzia saa moja na nusu jioni saa za Afrika Mashariki. Ukiwa hujabahatika kusikiliza matangazo ya siku yeyote ile, unaweza kuyasikiliza kwenye ukurasa wetu wa matangazo ya wiki. Sehemu ya pili ya matangazo unaweza kuyasikiliza kwenye sehemu ya vipindi vyetu hapo chini.

Bird Flu