Sauti ya Amerika  Swahili
Pata habari za kuaminika

Kwa Maandishi Pekee
Search

Radio Programs

Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika husikika kila siku - Jumatatu hadi Jumapili - kwa muda wa saa nzima kuanzia saa moja na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki na saa 12 na nusu jioni kwa saa za Afrika ya Kati. Katika nusu saa ya kwanza tunakuletea habari muhimu za dunia na ripoti kutoka kwa waandishi wetu walioko sehemu mbali mbali za dunia.

Sehemu ya pili ya matangazo yetu ina vipindi mbali mbali, kuanzia Ulimwengu wa michezo, Wanawake, Vijana hadi Muziki. Maelezo kamili juu ya vipindi hivyo yanafuata. 

Pia tuna matangazo ya nusu saa alfajiri na mchana kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa. 


**Unaweza kusikiliza vipindi vyetu hapa kwa kubonyeza siku unayotaka.**

JUMATATU Audio icon

JUMANNE Audio icon

JUMATANO Audio icon
Michezo -
1700-1710
 UTC, 0800 EAT
Ulimwengu wa Wanawake -
1700-1720 UTC, 0800 EAT 
Afya Yako -
1700-1710 UTC, 0800 EAT
Kipindi kinachosikika kila jumatatu kikiwa na ripoti juu ya matukio mbalimbali ya michezo hapa Marekani, Afrika mashariki na kwingineko duniani. Hiki ni kipindi kinachosikika kila siku ya Jumanne kuhusu maswala ya wanawake na watoto. Makala yanajadili matatizo na maendeleo ya wanawake na watoto kote duniani.Makala ya kipindi cha "Sayansi na Afya" hutangazwa kila siku ya jumatano, kinachomulika kwenye maswala ya ugunduzi wa kisayansi, kiteknolojia na tiba ya magonjwa mbali mbali. Kipindi hiki pia hutangaza mijadala na ripoti zinazohusu njia mpya za uboreshaji wa afya ya jamii hususani katika nchi zinazoendelea.
Amerika Leo -
1710-1720 UTC, 0810 EAT
Jamii na Manedeleo -
1710-1720 UTC, 0810 EAT
Muziki kutoka Afrika -
1710-1720 UTC, 0810 EAT
Kipindi hiki kinasikika kila siku ya jumatatu. Kinahusu maswala mbali mbali yanayotokea Marekani - maisha ya kila siku, siasa, uchumi na utamaduni.Kipindi cha "Kilimo Wiki Hii" kinachokujia kila siku ya jumanne. Waandishi wa Sauti ya Amerika wanachangia makala katika kipindi hiki kuhusu maendeleo na matatizo katika kilimo pamoja na mbinu mpya za kilimo hasa katika nchi zinazoendelea, na habari kuhusu ripoti za utafiti wa kilimo.Muziki wa kiafrika huwajieni kila siku ya jumatano. Ni kipindi kinachowaleteni muziki na mahojiano ya wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali za bara hilo.Tungelifurahi kupokea muziki  kutoka kwenu ili kuweza kuendelea kukuza muziki na wanamuziki wa Afrika.
ALHAMISI Audio iconIJUMAA Audio iconJUMAMOSI Audio icon
Matukio Afrika  -
1700-1710 UTC, 0800 EAT
Salamu na Muziki -
1710-1720 UTC, 0810 EAT
Maswali na Majibu -
1640 -1700 UTC, 0740 EAT
Kipindi kinachoelezea kwa kina na kwa uchambuzi matukio muhimu katika sehemu mbalimbali za bara la Afrika.Mahojiano na baadhi ya wahusika katika habari na maoni.Hiki ni kipindi cha salamu za wasikilizaji kutoka sehemu mbali mbali duniani ambako sauti ya America inasikika. Wasikilizaji huandika barua za salamu na maombi ya rekodi ambazo husomwa hewani zikiambatana na muziki motomoto.Maswali ya wasikilizaji hujibiwa kila siku ya jumamosi.Wasikilizaji hutuandikia kwa kutumia anwani  ya Swahili Service, Voice of America, C Street SW. Washintgton DC 20247. Au kwa kupitia anwani yetu ya voaswahili@voanews.com Masuali yanahusu kila kitu kuanzia maisha ya kawaida hadi uvumbuzi wa mambo mbali mbali sayansi hadi maisha ya mtu yeyote yule.
Vijimambo -
1710-1720 UTC, 0810 EAT
Ulimwengu wa Vijana-
1700-1710 UTC, 0800 EAT
JUMAPILI Audio icon
Hiki ni kipindi kinachokuletea orodha ya rekodi kumi bora za muziki hapa Marekani kila siku ya alhamisi, kulingana na uamuzi wa wahariri wa gazeti la Billboard la hapa Marekani ambalo linafuatilia umashuhuri wa rekodi za muziki. Hiki ni kipindi kinacho zungumzia maswala mbali mbali yanayo wahusu vijana. Kuanzia kuwapatia sauti katika maswala ya nchi hadi matatizo yanayowakumba katika maisha yao ya kila siku.Jarida la Jumapili -
1640-1700 UTC, 0740 EAT

yanayochambua kwa undani zaidi mambo yanayotokea katika maeneo yetu ya matangazo hasa huko Afrika Mashariki na ya Kati. Na yanazingatia maswala ambayo hayapati nafasi kuzungumziwa katika sehemu nyingine za vipidi vyetu kutokana na muda.